Friday, September 10, 2010
   
Text Size

Site Search

Aliyemvamia Kaka bado asota rumande

Na Tumain Kyomo, DACICO

JESHI la Polisi linaendelea kumshikilia shabiki wa soka ambaye juzi alivamia uwanja na kwenda kumkumbatia Ricardo Kaka wa Brazil ilipokuwa ikiumana na Taifa Stars.
Tukio hilo lililoshangaza wengi lilitokea Uwanja wa Taifa katika mechi hiyo ya kimataifa ya kirafiki, ambapo Stars ilichapwa mabao 5-1.

Kamanda wa Polisi wa Temeke, David Misime, alisema jana kuwa jeshi lake linamshikilia shabiki huyo, Ally Komba (21) ili kumhoji zaidi katika uchunguzi wa suala hilo.
Alisema mahojiano ya awali yanaonyesha Ally ni mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Green Acres ya jijini Dar es Salaam.


Wakati mechi hiyo iliyovuta hisia za mashabiki wengi nchini ikiendelea, shabiki huyo alichomoka ghafla ya kuingia uwanjani na kwenda kumkumbatia mshambuliaji huyo nyota.


Kwa mujibu wa kanuni za soka, shabiki yeyote haruhusiwi kuingia na kuwakaribia wachezaji katika sehemu ya kuchezea wakati mchezo ukiendelea.
Hata hivyo haikueleweka shabiki huyo alivukaje hadi kuingia uwanjani, kwani askari wa ulinzi walikuwapo.


More Latest News

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4

cartoons



Who's Online

We have 8 guests online

Login Form