Tuesday, September 07, 2010
   
Text Size

Site Search

Arobaini za madereva teksi Mbezi Luis zaja

Na Gabriel Mushi

SERIKALI ya Mtaa wa Mbezi Luis, imetoa onyo kwa madereva teksi wa kituo hicho kuacha tabia ya kuwatoza ushuru wafanyabiashara wadogo wadogo ‘wamachinga’ wanaofanya biashara kituoni hapo.

Akizungumza na Mtazania jana, Mwenyekiti wa Mtaa huo, Omari Mshauri alisema ingawa wafanyabishara hao hawatakiwi kufanya biashara kituoni hapo, lakini pia madereva teksi nao hawatakiwi kuwatoza ushuru.

“Nasikia kuwa kuna kinara wa madereva hao anaeitwa Geradi ambapo anawatoza ushuru wa Sh 500 kila kichwa kila siku huku akifahamu kuwa kufanya hivyo kinyume na sheria. Hii sio sahihi. Sisi tulikaa na wafanyabiashara hao, madereva teksi na wakazi wenye nyumba karibu na kituo hiki tukakubaliana kuwa wafanyabishara hao wanatakiwa kulipa ushuru wa kuzoa takataka pekee.

“Lakini pia nasikia wafanyabiashara hao wamekuwa wakitishiwa na madereva hao kutolewa kituoni hapo wasipokuwa wakilipa ushuru huo mwingine. Hili ni jambo ambalo tutaanza kulichukulia hatua muda si mrefu,” alisema.

Hatua hii imekuja kutokana na baadhi ya wakazi waliopo karibu na kituo hicho kulalamikia hatua ya madereva hao kujiidhinishia hatua ya kuwatoza wafanyabiashara hao ushuru.

Mmoja wa wakazi hao, Chiku Sungura, mwenye nyumba iliyopo karibu na kituo hicho alisema awali alikuwa akichukua ushuru kwa baadhi ya wafanyabiashara hao wanaofanya biashara pembezoni mwa nyumba yake, ila mambo yamebadilika.

“Lakini sasa huyu Kinara wa Madereva teksi, Gerad amekuwa akitumia nguvu na kujiamulia kuchukua ushuru wakati akifahamu wanaofanya biashara kwenye viambaza vya nyumba zetu wanatakiwa kutulipa sisi.

“Tunafahamu kuwa sisi wenye nyumba za karibu hapa pia tunatakiwa kuhama lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa katika kutufidia kwa maana bado tunayo mamlaka ya kuchukua ushuru kwa wale wanaofanya biashara kwenye nyumba nyumba zetu,” alisema.

Kinara wa madereva teksi hao, Gerad alikana kuwatoza ushuru wafanyabiashara hao na kusema kuwa huwa wanawaachia kufanya biashara zao bila kuwatoza ushuru wowote.



More Latest News

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4

cartoons



Who's Online

We have 17 guests online

Login Form