Tuesday, September 07, 2010
   
Text Size

Site Search

KKKT wamtetea Rais Kikwete

a Audax Mutiganzi, Bukoba

KANISA la Kiinjili la Kilutheli Tanzana (KKKT) Dayosisi Kaskazini Magharibi, limemtetea Rais jakaya Mrisho Kikwete dhidi ya tuhuma zilizoelekezwa kwake na Gazeti la Mwana halisi Toleo Na 194 la Juni 23-29, mwaka huu.

Taarifa iliyolewa na Askofu wa Dayosisi hiyo Elisa Buberwa kwa vyombo vya habari mwishoni mwa wiki ilipinga vikali taarifa iliyoandikwa kwenye gazeti hilo iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho “Maaskofu wamem’gunikia Rais Kikwete.”

Buberwa aliwaambia waandishi wa habari lilizoandika gazeti hilo kuwa Rais Kikwete alikataa kuhudhuria ibada na alikataa kula chakula na maaskofu walioudhuria maadhimisho hayo kulingana na ratiba ilivyokuwa zilikuwa za uongo na zinalenga kuleta chuki kati ya Kanisa hilo na Rais Kikwete.

Alisema Rais Kikwete alipofika mkoani Kagera kuhudhuria maadhimisho hayo akitokea kwenye mikoa mbalimbali, ambapo alikuwa anaendelea na ziara za kiserikali, aliuomba
uongozi wa kanisa hilo ubadili ratiba kidogo na uongozi uliridhia maombi hayo.

Buberwa aliyekuwa ameandamana na Katibu Mkuu wa KKKT, Godwin Lwezaura, alisema Rais Kikwete aliomba udhuru wa kutohudhuria ibada ya kilele cha sherehe za maadhimisho ya miaka 100 kwa kuwa alikuwa amechoka kutokana na ziara za mfululizo alizozifanya kwenye mikoa mbalimbali.

Alisema muda aliofika wa saa 7:00 kwenye viwanja vya Kashura kuhudhuria maadhimisho hayo na kukuta baadhi ya wageni mbalimbali toka duniani kote wanatoa salamu mbalimbali ulikuwa umepangwa iwe hivyo.

Kuhusu suala la kutokula na maaskofu, Buberwa alifafanua maaskofu wa kanisa hilo wachelewa kuingia kwenye ukumbi. Aliongeza kuwa kuchelewa kwa maaskofu hao
kulimlazimisha Rais apande ndege bila kula kwa kuwa ratiba yake
ilikuwa finyu na siku hiyo alikuwa anatakiwa mkoani Dodoma kufanya
maandalizi ya kuchukua fomu ya kuwania urais.


More Latest News

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4

cartoons



Who's Online

We have 13 guests online

Login Form