Tuesday, September 07, 2010
   
Text Size

Site Search

Daladala latumbukia mtoni Dar

ABIRIA 21 waliokuwa wakisafiri kutoka Buguruni kwenda Mbagala jijini Dar es Salaam, jana walinusurika kifo baada ya daladala walilokuwamo kuacha njia na kutumbukia katika Mto Kizinga, uliopo Mtoni Mtongani.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Mkuu wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, ACP Daniel Misime, alisema ajali hiyo ilitokea saa nane mchana na kuhusisha gari aina ya Toyota Coaster, lenye namba za usajili T 323 BEB, lililokuwa likiendeshwa na Shabani Msafiri, Mkazi wa Yombo Kilakala.

Misime alisema chanzo cha ajali hiyo ni kupasuka kwa gurudumu na kwa kuwa lilikuwa katika mwendo kasi, lilimshinda dereva likagonga nguzo za daraja na kutumbukia mtoni.

Majeruhi 18 walikimbizwa katika Hospitali ya Temeke kwa ajili ya matibabu, ambapo 14 kati yao walitibiwa na kuruhusiwa kuondoka, huku wengine watatu wakihamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya hali zao kuwa mbaya.

Muuguzi wa zamu wa hospitali hiyo, Neema Beda, alisema majeruhi mmoja alibakizwa hospitalini hapo kwa uangalizi zaidi, huku wengine watatu wakijitokeza baadaye na kudai kuwa wao ni miongoni mwa waliokuwamo katika ajali hiyo.

Majeruhi waliokimbizwa Muhimbili ni Sinai Selemani, Amina Shomari na Omari Said, wakati aliyebakizwa hospitali ya Temeke ni Stumai Rajabu, mkazi wa Mbagala Rangi Tatu.

Waliotibiwa na kuruhusiwa ni pamoja na Mwajuma Hamis, Rehema Ramadhan, Maria Hassan, Janeth James, Salima Salehe, Tabu Zuberi na Fikira Awadhi. Wengine ni Omari Micheyo, Pili Mohamedi na Slami Abdalah.

More Latest News

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4

cartoons



Who's Online

We have 14 guests online

Login Form