Tuesday, September 07, 2010
   
Text Size

Site Search

CCM waanza kazi rasmi

*Waziri Mkuu Pinda apita bila kupingwa Rukwa
*Igunga watoa kali, wamchukulia Rostam fomu
*Aheshimu wananchi, aijaza na kuirejesha jana
*Fomu ya Dk Makongoro Mahanga yakubaliwa
*Kampeni zaanza rasmi leo, wagombea gari moja

Waandishi Wetu, Dar na mikoani

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, amekuwa mgombea pekee ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya kubainika kuwa amechukua na kurejesha fomu peke yake ya kuomba kupigiwa kura za maoni kugombea ubunge katika Jimbo la Mlele.

Hali hiyo ilibainika jana saa 10 jioni ambapo ndiyo ulikuwa mwisho wa kuchukua fomu na kurejesha. Katibu wa CCM, Wilaya ya Mpanda, Mohamed Nyawenga, alimtangaza Pinda kuwa mgombea pekee na kuwa amepita bila kupingwa ndani ya CCM kutetea kiti hicho katika uchaguzi wa Oktoba.

Akirejesha fomu hiyo jana, Pinda alikemea tabia ya rushwa katika chaguzi za ndani ya CCM zilizoanza kuibuka kutokana na kuchukua na kurejesha fomu za kuomba kupigiwa kura ya maoni kwa wagombea.

Akizungumza na wana CCM waliojitokeza kumsindikiza kurejesha fomu yake, Pinda alisema: “Sheria mpya ya uchaguzi inakataza vitendo vya rushwa kwa wagombea wote katika ngazi zote, ikiwa ni pamoja na kwa wanachama kuomba rushwa.”

Pinda ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu, alisema CCM imejipanga kupambana na rushwa ya aina yoyote katika kura ya maoni wapatikane wagombea waadilifu watakaokipa chama ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu.

“Atayekuwa amepatikana akitoa au kuomba rushwa ni dhahiri kuwa hatapitishwa na vikao vya chama,” alisema Pinda.

Waziri Mkuu pia aliwataka wagombea wote waliojaza fomu za kuomba kupigiwa kura ya maoni kukubali matokeo kutokana na ukweli kwamba waliochukua fomu ni wengi na anayetakiwa kuteuliwa ni mmoja tu.

Jimbo la Igunga

Wakazi wa Jimbo hili jana walitoa kali kwa kuamua kuchukua fomu kwa ajili ya Rostam Aziz jana asubuhi na kumtaka aende kuijaza, hivyo akalazimika kutii maombi yao. Rostam alikuwa amesisitiza kuwa hagombei tena ubunge, lakini hatua waliyochukua wazee wa Tabora na hasa Jimbo la Igunga, imemfanya aheshimu mawazo yao na kujaza fomu hiyo akiwa katika Ofisi za CCM Igunga akairejesha.
Hadi saa kumi jana jioni walikuwa wamejitokeza wagombea wengine 9 kuomba wateuliwe kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Igunga.
Ashindwa kurejesha fomu Kinondoni

MGOMBEA mmoja kati ya wagombea 38 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliochukua fomu za kuwania Ubunge katika Wilaya ya Kinondoni yenye majimbo matatu ya Ubungo, Kawe na Kinondoni, ameshindwa kurejesha fomu yake.

Akizungumza na Mtanzania Dar es Salaam jana, Katibu Msaidizi Mkuu ambaye pia ni Mhasibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Abihudi Shilla, alisema hadi kufikia jana saa 10 jioni, Godwin Kamala alikuwa hajarejesha fomu hiyo.

Waliorejesha fomu Jimbo la Ubungo

Shamsa Mwangunga, Nape Nnauye, Dk. Apollo  Kissai, Slaus Mwishemba, Col. Gaspar Hiza, Alfred Nchimbi, Peter Msuya, Hawa Mg’humbi, Assumpta Nalitolea, Michael Lupiana, Perpetua Haule na Eliona Nkya.

Jimbo la Kawe

Faustin Kikove, Mahamoud Madenge, Nicodemus Chengula, Eric Suma, Omari Wahure, Biton Mwenisongole, Harold Maruma, Dk. Malima Bundara, Jumaa Pijei, Margaret Lema, Japhet Robi, Angela Kizigha, Dk. Petronilla Ngiloi, Elias Nasera, Zainuddin Adamjee na Kippi Warioba.

Jimbo la Kinondoni

Iddi Azzan, Mustafa Muro, Kakolwa Mbano, Shy-Rose Bhanji, Issa Omary, Godwin Kabisa, Mpoki Mwambulukutu, Bakari Maige, Mateo Kanela na Mackdonald Lunyilija.

Wakati huo huo, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Kinondoni, Sahah Mgoli, alisema kuwa wagombea wote wa Ubunge Viti Maalumu Mkoa wamerejesha fomu zao kwa wakati.

Aliwataja kuwa Zarina Madabida, Tatu Malyaga, Margaret Kimambo, Grace Mtesigwa, Amina Israel, Mossy Mbwando, Hadija Kopa, Joyce Kajula na Nuru Kaku.

Katika mkutano wa pamoja wa wagombea, Katibu wa CCM wa Wilaya ya Kinondoni, Mwalimu Godfrey Tondo, aliwaasa wagombea wote wafanye siasa za kueleza sera zao na si kupakana matope. Alisema baada ya kampeni hizo atapatikana mshindi mmoja ambaye wote watampigia debe kukinadi CCM.

Aliwambia wagombea hao hawaruhusiwi kuweka mabango wala kutoa rushwa, na kwamba atakayekwenda kwenye kata kupiga kampeni usiku au akaficha wapigakura atafutwa kwenye kinyang’anyiro hicho.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Aron Mwaikambo, alisema mgombea kuwa wa kwanza kwenye kura za maoni si mwisho wa ushindani kwani Chama kinaweza kuona anapungukiwa baadhi ya sifa na kikaamua kumwacha pembeni mshindi wa kwanza akachukuliwa hata mshindi wa nne.

Mwenyekiti huyo alisema hata kama mgombea hataki kutumia gari la pamoja atalazimika kuchangia Sh milioni moja itakayotumika kuandaa mikutano ya hadhara.

Udiwadi Ubungo

Sophia Fitina, Joan Mazanda, Elukaga Minango, Angela Mfinanga, Asnath Mambo, Florence Masunga, Tatu Mnekeya, Angela Halla, Theresia Chihota, Zuena Abdallah, Grace Kabigi, Salama Lusogo, Ningile Kapange, Ester Mkandawile, Omega Masawe, Nuru Kaku na Rehema Mayunga.

Jimbo la Kawe

Hilda Rwebangira, Kulthum Sagamiko, Everly Hatibu, Bernadette Ritti, Mwanaisha Sudi, Rozina Urio, Renata Semitende, Julia Hoza, Leah Onyango, Asha Majura na Basilisa Sawere.

Jimbo la Kinondoni

Grace Mwashala, Hilda Rwezaura, Kimwana Sherally, Lilian Mchaa, Florence Ndege, Subira Kondo, Huba Hassan, Tiba Hamisi na Fatma Salim.

Jimbo la Ukonga

Waliorudisha fomu hadi kufikia saa 7 mchana jana, ni Godwin Barongo, Hamza Abdallah, Aziza Mwalusali, Mnanga Selelya, Chacha Wambura, Sande Mnozya, Eugen Mwaioposa, Beatrice Moses Kabonyoka na Issaya Christabella.

Jimbo la Ilala

Mussa Azan Zungu na Jafari Juma.

Jimbo la Segerea

Dk. Makongoro Mahanga, Salusian Kato, Kiomoni Kibamba, Glorious Luoga, Paul Mahondo, John Jambele, Joseph Kessy na Venance Victor.

Kutoka Mbeya

Wagombea ubunge 14 kati ya 19, waliochukua fomu za kugombea ubunge katika Majimbo ya Mbeya Mjini na Mbeya vijijini kupitia CCM, wamerudisha fomu zao.

Mbeya Mjini

Waliorudisha fomu ni Michael Mwandumbya, Maria Mwambanga, Uugen Kasonga, Frank Mwaisumbe, Benson Mpesya, Franco Mwalutende, Thom Mwang’onda, Meshaki Kapange na Felix Mbogela.

Mbeya Vijijini

Andrew Saile, Michael Mponzi, Kassim Chakachaka, Petro Mwashusa na Dikson Sinkwembe.

Rushwa Dodoma

Mchakato wa kuwania nafasi za ubunge Dodoma umezua balaa katika Wilaya ya Kondoa, kutokana na baadhi ya wapambe wa mgombea ubunge Jimbo la Kondoa Kaskazini (jina linahifadhiwa), kudaiwa kutoa rushwa kwa wananchi.

Rushwa inayodaiwa kutolewa na mgombea huyo ni pamoja na fulana na fedha hali iliyosababisha kila mtu kushangazwa na kitendo hicho. Mtanzania ilipata taarifa hizo kwa nyakati tofauti kutoka kwa watu mbalimbali ambao walikataa kutaja majina yao. Hata hivyo, Katibu wa CCM Wilaya ya Kondoa, Everlin Jordan, alikanusha kuwapo kwa taarifa hizo.

Kimbisa Kivukoni

MEYA wa Jiji la Dar es Salaamu, Adamu Kimbisa, amekanusha kuchukua fomu ya udiwani kutetea Kata yake ya Kivukoni.

Kimbisa ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, kupitia Mkoa wa Dodoma, alikanusha kuchukua fomu ya udiwani jana, wakati akichukua fomu ya ubunge wa Jimbo la Dodoma mjini.

Alisema si kweli kwamba amechukua fomu ya udiwani bali hizo ni porojo za uchaguzi. “Sio kweli kuwa nimechukua fomu ya kugombea udiwani isipokuwa hizo ni porojo za uchaguzi,” alisema Kimbisa.

Katibu wa CCM wa Wilaya ya Dodoma Mjini, David Mzuri, alisema hadi jana saa 6 mchana tayari wanachama 19
walikuwa wameshachukua fomu katika Jimbo la Dodoma Mjini huko baadhi walionekana wakirejesha fomu.

Jimbo la Buchosa

Mwalimu wa Ujasiriamali na Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Eric James Shigongo, jana alikuwa mmoja wa wanachama waliorejesha fomu za kuomba uteuzi wa kuwania ubunge katika Uchaguzi Mkuu 2010.

Shigongo alirejesha fomu yake jana mchana kwenye ofisi ya CCM, Sengerema na kupokewa na Katibu wa chama hicho wa wilaya, Michael Kahuruda.

Akirudisha fomu hiyo Shigongo alisema ameamua kujitosha kuwania ubunge Buchosa kwa sababu siyo tu kwamba ameombwa na wazee na wananchi wengine, bali pia amejipanga kutoa tiba kwa matatizo sugu yaliyomo jimboni humo.

Kutoka Iringa Mjini

Frederick Mwakalebela ni miongoni mwa wagombea 12, waliorejesha fomu jana kugombea ubunge katika jimbo hilo. Mwakalebela anagombea Jimbo la Iringa Mjini ambalo kwa sasa linashikiliwa na Monica Mbega.

Udiwani Bunda

Joseph Malimbe

Arusha warejesha fomu kimya kimya

Wagombea ubunge kwa tiketi ya CCM waliochukua fomu za kugombea ubunge Mjini Arusha, wamerudisha fomu zao katika ofisi za wilaya hapa mjini kimya kimya. Miongoni mwa waliorudisha fomu hizo jana ni pamoja na Dk. Batilda Buriani na Dk. Hamisi Kibola huku wagombea wengine wakiwa bado wanasubiriwa. Wagombea wengine waliochukua fomu na kuzirejesha ni pamoja na Deogratius Mtui, Felix Mrema na Micheal Sekajingo.

Jimbo la Ngorongoro

Mathewtak  Ole  Timan, Saning Ole Telele, Fidelis Ole Kashy, Godfrey Laliya, William Ole Nasha, Pius Sanai, Peter Metele, Vicent Mbirika  na  Patrick Gwedig nako  Wilaya ya Karatu ni John Burra, Dk Lorry na Dk Sixbert.

Jimbo la Monduli

Waziri Mkuu (mstaafu) Edward Lowassa, Dk. Salash Toure, Wilaya ya Arumeru Magharabi ni Goodluck ole Medeye, Elisa Mollel na Thomas Sabaya.

Arumeru Mashariki

William Sarakikya, Anthony Musani, Elirehema Kaaya na Jeremia Sumari.

 

More Latest News

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4

cartoons



Who's Online

We have 15 guests online

Login Form