AG: Mawaziri bado ni mawaziri
Na Mwandishi Wetu
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, ametoa ufafanuzi kuwa mawaziri wote wanaendelea kushika nyadhifa zao hadi muda mfupi kabala ya Rais Mteule kuapishwa.
Jaji Werema alitoa ufafanuzi huo Dar es Salaam jana, baada ya vyombo mbalimbali vya habari kuchapisha habari na makala vikionyesha kuwa baada ya Bunge kuvunjwa, mawaziri wanapoteza sifa za kuwa mawaziri hivyo kazi zote za Serikali zitaendeshwa na makatibu wakuu.
Kifungu cha 57 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kinaeleza mazingira saba ya kuvunjwa kwa Baraza la Mawaziri linalowahusisha Makamu wa Rais, Rais wa Zanzibar na mawaziri wengine, na kinaweka wazi katika sehemu ya B inayoonyesha kuwa kuvunjwa kwa Bunge hakuhusiani na kuvunjwa kwa Baraza la Mawaziri.
Kwa mujibu wa kifungu hicho cha 57 (2) (b), waziri atapoteza uwaziri wake ikiwa mwenye madaraka hayo atakoma kuwa mbunge kwa sababu yoyote isiyohusika na kuvunjwa kwa Bunge.
“Kwa kuzingatia masharti mbalimbali yaliyomo katika Katiba, kuvunjwa kwa Bunge hakusababishi kuwepo kwa ombwe la uongozi wa nchi. Baraza la Mawaziri litaendelea kuwapo na linaweza kukutana wakati wowote. Hali kadhalika, Rais na Makamu wa Rais wataendelea kutekeleza majukumu yao ya kikataiba au kisheria.
“Vile vile, kwa niaba ya Rais, shughuli zote za utendaji za Serikali, zitaendelea kutekelezwa na watumishi wa Serikali kama ilivyoainishwa katika Ibara ya 35 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Jaji Werema katika taarifa hiyo yenye kurasa tano.
More Latest News
-
Daladala latumbukia mtoni Dar ABIRIA 21 waliokuwa wakisafiri kutoka Buguruni kwenda Mbagala jijini...
-
Umeyasikia ya Tatu Ntimizi? BAADHI ya wananchi wa Jimbo la Igalula ambao ni wanachama wa Chama...
-
Hispania yaweka historia HISPANIA imekuwa taifa la nane kushinda Kombe la Dunia baada...
- 1
- 2
- 3
- 4
Advertisement

cartoons


