Friday, September 10, 2010
   
Text Size

Site Search

mtanzania

AG: Mawaziri bado ni mawaziri

Na Mwandishi Wetu

MWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, ametoa ufafanuzi kuwa mawaziri wote wanaendelea kushika nyadhifa zao hadi muda mfupi kabala ya Rais Mteule kuapishwa.

Jaji Werema alitoa ufafanuzi huo Dar es Salaam jana, baada ya vyombo mbalimbali vya habari kuchapisha habari na makala vikionyesha kuwa baada ya Bunge kuvunjwa, mawaziri wanapoteza sifa za kuwa mawaziri hivyo kazi zote za Serikali zitaendeshwa na makatibu wakuu.

Kifungu cha 57 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kinaeleza mazingira saba ya kuvunjwa kwa Baraza la Mawaziri linalowahusisha Makamu wa Rais, Rais wa Zanzibar na mawaziri wengine, na kinaweka wazi katika sehemu ya B inayoonyesha kuwa kuvunjwa kwa Bunge hakuhusiani na kuvunjwa kwa Baraza la Mawaziri.

Kwa mujibu wa kifungu hicho cha 57 (2) (b), waziri atapoteza uwaziri wake ikiwa mwenye madaraka hayo atakoma kuwa mbunge kwa sababu yoyote isiyohusika na kuvunjwa kwa Bunge.

“Kwa kuzingatia masharti mbalimbali yaliyomo katika Katiba, kuvunjwa kwa Bunge hakusababishi kuwepo kwa ombwe la uongozi wa nchi. Baraza la Mawaziri litaendelea kuwapo na linaweza kukutana wakati wowote. Hali kadhalika, Rais na Makamu wa Rais wataendelea kutekeleza majukumu yao ya kikataiba au kisheria.

“Vile vile, kwa niaba ya Rais, shughuli zote za utendaji za Serikali, zitaendelea kutekelezwa na watumishi wa Serikali kama ilivyoainishwa katika Ibara ya 35 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Jaji Werema katika taarifa hiyo yenye kurasa tano.

 

Moto wawaka CCM

*Shangingi la mbunge lachomwa moto
*Viongozi watano CCM wasimamishwa
*Mtambo wa kufyatua kadi wakamatwa
*Wabunge 8 Mwanza wapumulia mashine
*Shy-Rose ampeleka puta Azzan Kinondoni
*Makalla, Murad moto, Ubungo ni kizaazaa

Waandishi Wetu, mikoani na Dar

MOTO unazidi kuwaka ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo watu wawili wameuawa kwa kugongwa na gari la mbunge wa Musoma Vijijini aliyemaliza muda wake, Nimrod Mkono, katika eneo la Mkiringo, Barabara ya Musoma-Mwanza.

Kama kulipiza kisasi, kwa hasira wananchi waliofika eneo la tukio nao wameamua kulichoma moto shangingi la mbunge huyo na kuliteketeza kabisa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, ACP Robert Boaz, alisema tukio hilo lilitokea saa 2 usiku. Gari lililohusika ni lenye namba T 173 AZW aina ya Nissan Patrol, lililokuwa likitoka Mjini Musoma kwenda kijijini Busegwe ambako ndiko nyumbani kwa Mkono.

Alisema wakati wa tukio, Mkono hakuwamo kwenye gari hilo. Lilikuwa likiendeshwa na Petro Andrea (43).

Kamanda Boaz alisema waliokufa walikuwa katika pikipiki. Walitambuliwa kuwa ni Magori Magori (39), aliyekuwa akiendesha pikipiki na Wambura Kitongori (40). Wote ni wakazi wa Nyabange, wilayani Musoma.

 

CCM waanza kazi rasmi

*Waziri Mkuu Pinda apita bila kupingwa Rukwa
*Igunga watoa kali, wamchukulia Rostam fomu
*Aheshimu wananchi, aijaza na kuirejesha jana
*Fomu ya Dk Makongoro Mahanga yakubaliwa
*Kampeni zaanza rasmi leo, wagombea gari moja

Waandishi Wetu, Dar na mikoani

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, amekuwa mgombea pekee ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya kubainika kuwa amechukua na kurejesha fomu peke yake ya kuomba kupigiwa kura za maoni kugombea ubunge katika Jimbo la Mlele.

Hali hiyo ilibainika jana saa 10 jioni ambapo ndiyo ulikuwa mwisho wa kuchukua fomu na kurejesha. Katibu wa CCM, Wilaya ya Mpanda, Mohamed Nyawenga, alimtangaza Pinda kuwa mgombea pekee na kuwa amepita bila kupingwa ndani ya CCM kutetea kiti hicho katika uchaguzi wa Oktoba.

Akirejesha fomu hiyo jana, Pinda alikemea tabia ya rushwa katika chaguzi za ndani ya CCM zilizoanza kuibuka kutokana na kuchukua na kurejesha fomu za kuomba kupigiwa kura ya maoni kwa wagombea.

Akizungumza na wana CCM waliojitokeza kumsindikiza kurejesha fomu yake, Pinda alisema: “Sheria mpya ya uchaguzi inakataza vitendo vya rushwa kwa wagombea wote katika ngazi zote, ikiwa ni pamoja na kwa wanachama kuomba rushwa.”

Pinda ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu, alisema CCM imejipanga kupambana na rushwa ya aina yoyote katika kura ya maoni wapatikane wagombea waadilifu watakaokipa chama ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu.

“Atayekuwa amepatikana akitoa au kuomba rushwa ni dhahiri kuwa hatapitishwa na vikao vya chama,” alisema Pinda.

Waziri Mkuu pia aliwataka wagombea wote waliojaza fomu za kuomba kupigiwa kura ya maoni kukubali matokeo kutokana na ukweli kwamba waliochukua fomu ni wengi na anayetakiwa kuteuliwa ni mmoja tu.

Jimbo la Igunga

Wakazi wa Jimbo hili jana walitoa kali kwa kuamua kuchukua fomu kwa ajili ya Rostam Aziz jana asubuhi na kumtaka aende kuijaza, hivyo akalazimika kutii maombi yao. Rostam alikuwa amesisitiza kuwa hagombei tena ubunge, lakini hatua waliyochukua wazee wa Tabora na hasa Jimbo la Igunga, imemfanya aheshimu mawazo yao na kujaza fomu hiyo akiwa katika Ofisi za CCM Igunga akairejesha.
Hadi saa kumi jana jioni walikuwa wamejitokeza wagombea wengine 9 kuomba wateuliwe kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Igunga.
Ashindwa kurejesha fomu Kinondoni

MGOMBEA mmoja kati ya wagombea 38 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliochukua fomu za kuwania Ubunge katika Wilaya ya Kinondoni yenye majimbo matatu ya Ubungo, Kawe na Kinondoni, ameshindwa kurejesha fomu yake.

Akizungumza na Mtanzania Dar es Salaam jana, Katibu Msaidizi Mkuu ambaye pia ni Mhasibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Abihudi Shilla, alisema hadi kufikia jana saa 10 jioni, Godwin Kamala alikuwa hajarejesha fomu hiyo.

Waliorejesha fomu Jimbo la Ubungo

Shamsa Mwangunga, Nape Nnauye, Dk. Apollo  Kissai, Slaus Mwishemba, Col. Gaspar Hiza, Alfred Nchimbi, Peter Msuya, Hawa Mg’humbi, Assumpta Nalitolea, Michael Lupiana, Perpetua Haule na Eliona Nkya.

Jimbo la Kawe

Faustin Kikove, Mahamoud Madenge, Nicodemus Chengula, Eric Suma, Omari Wahure, Biton Mwenisongole, Harold Maruma, Dk. Malima Bundara, Jumaa Pijei, Margaret Lema, Japhet Robi, Angela Kizigha, Dk. Petronilla Ngiloi, Elias Nasera, Zainuddin Adamjee na Kippi Warioba.

Jimbo la Kinondoni

Iddi Azzan, Mustafa Muro, Kakolwa Mbano, Shy-Rose Bhanji, Issa Omary, Godwin Kabisa, Mpoki Mwambulukutu, Bakari Maige, Mateo Kanela na Mackdonald Lunyilija.

Wakati huo huo, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Kinondoni, Sahah Mgoli, alisema kuwa wagombea wote wa Ubunge Viti Maalumu Mkoa wamerejesha fomu zao kwa wakati.

Aliwataja kuwa Zarina Madabida, Tatu Malyaga, Margaret Kimambo, Grace Mtesigwa, Amina Israel, Mossy Mbwando, Hadija Kopa, Joyce Kajula na Nuru Kaku.

Katika mkutano wa pamoja wa wagombea, Katibu wa CCM wa Wilaya ya Kinondoni, Mwalimu Godfrey Tondo, aliwaasa wagombea wote wafanye siasa za kueleza sera zao na si kupakana matope. Alisema baada ya kampeni hizo atapatikana mshindi mmoja ambaye wote watampigia debe kukinadi CCM.

Aliwambia wagombea hao hawaruhusiwi kuweka mabango wala kutoa rushwa, na kwamba atakayekwenda kwenye kata kupiga kampeni usiku au akaficha wapigakura atafutwa kwenye kinyang’anyiro hicho.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Aron Mwaikambo, alisema mgombea kuwa wa kwanza kwenye kura za maoni si mwisho wa ushindani kwani Chama kinaweza kuona anapungukiwa baadhi ya sifa na kikaamua kumwacha pembeni mshindi wa kwanza akachukuliwa hata mshindi wa nne.

Mwenyekiti huyo alisema hata kama mgombea hataki kutumia gari la pamoja atalazimika kuchangia Sh milioni moja itakayotumika kuandaa mikutano ya hadhara.

Udiwadi Ubungo

Sophia Fitina, Joan Mazanda, Elukaga Minango, Angela Mfinanga, Asnath Mambo, Florence Masunga, Tatu Mnekeya, Angela Halla, Theresia Chihota, Zuena Abdallah, Grace Kabigi, Salama Lusogo, Ningile Kapange, Ester Mkandawile, Omega Masawe, Nuru Kaku na Rehema Mayunga.

Jimbo la Kawe

Hilda Rwebangira, Kulthum Sagamiko, Everly Hatibu, Bernadette Ritti, Mwanaisha Sudi, Rozina Urio, Renata Semitende, Julia Hoza, Leah Onyango, Asha Majura na Basilisa Sawere.

Jimbo la Kinondoni

Grace Mwashala, Hilda Rwezaura, Kimwana Sherally, Lilian Mchaa, Florence Ndege, Subira Kondo, Huba Hassan, Tiba Hamisi na Fatma Salim.

Jimbo la Ukonga

Waliorudisha fomu hadi kufikia saa 7 mchana jana, ni Godwin Barongo, Hamza Abdallah, Aziza Mwalusali, Mnanga Selelya, Chacha Wambura, Sande Mnozya, Eugen Mwaioposa, Beatrice Moses Kabonyoka na Issaya Christabella.

Jimbo la Ilala

Mussa Azan Zungu na Jafari Juma.

Jimbo la Segerea

Dk. Makongoro Mahanga, Salusian Kato, Kiomoni Kibamba, Glorious Luoga, Paul Mahondo, John Jambele, Joseph Kessy na Venance Victor.

Kutoka Mbeya

Wagombea ubunge 14 kati ya 19, waliochukua fomu za kugombea ubunge katika Majimbo ya Mbeya Mjini na Mbeya vijijini kupitia CCM, wamerudisha fomu zao.

Mbeya Mjini

Waliorudisha fomu ni Michael Mwandumbya, Maria Mwambanga, Uugen Kasonga, Frank Mwaisumbe, Benson Mpesya, Franco Mwalutende, Thom Mwang’onda, Meshaki Kapange na Felix Mbogela.

Mbeya Vijijini

Andrew Saile, Michael Mponzi, Kassim Chakachaka, Petro Mwashusa na Dikson Sinkwembe.

Rushwa Dodoma

Mchakato wa kuwania nafasi za ubunge Dodoma umezua balaa katika Wilaya ya Kondoa, kutokana na baadhi ya wapambe wa mgombea ubunge Jimbo la Kondoa Kaskazini (jina linahifadhiwa), kudaiwa kutoa rushwa kwa wananchi.

Rushwa inayodaiwa kutolewa na mgombea huyo ni pamoja na fulana na fedha hali iliyosababisha kila mtu kushangazwa na kitendo hicho. Mtanzania ilipata taarifa hizo kwa nyakati tofauti kutoka kwa watu mbalimbali ambao walikataa kutaja majina yao. Hata hivyo, Katibu wa CCM Wilaya ya Kondoa, Everlin Jordan, alikanusha kuwapo kwa taarifa hizo.

Kimbisa Kivukoni

MEYA wa Jiji la Dar es Salaamu, Adamu Kimbisa, amekanusha kuchukua fomu ya udiwani kutetea Kata yake ya Kivukoni.

Kimbisa ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, kupitia Mkoa wa Dodoma, alikanusha kuchukua fomu ya udiwani jana, wakati akichukua fomu ya ubunge wa Jimbo la Dodoma mjini.

Alisema si kweli kwamba amechukua fomu ya udiwani bali hizo ni porojo za uchaguzi. “Sio kweli kuwa nimechukua fomu ya kugombea udiwani isipokuwa hizo ni porojo za uchaguzi,” alisema Kimbisa.

Katibu wa CCM wa Wilaya ya Dodoma Mjini, David Mzuri, alisema hadi jana saa 6 mchana tayari wanachama 19
walikuwa wameshachukua fomu katika Jimbo la Dodoma Mjini huko baadhi walionekana wakirejesha fomu.

Jimbo la Buchosa

Mwalimu wa Ujasiriamali na Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Eric James Shigongo, jana alikuwa mmoja wa wanachama waliorejesha fomu za kuomba uteuzi wa kuwania ubunge katika Uchaguzi Mkuu 2010.

Shigongo alirejesha fomu yake jana mchana kwenye ofisi ya CCM, Sengerema na kupokewa na Katibu wa chama hicho wa wilaya, Michael Kahuruda.

Akirudisha fomu hiyo Shigongo alisema ameamua kujitosha kuwania ubunge Buchosa kwa sababu siyo tu kwamba ameombwa na wazee na wananchi wengine, bali pia amejipanga kutoa tiba kwa matatizo sugu yaliyomo jimboni humo.

Kutoka Iringa Mjini

Frederick Mwakalebela ni miongoni mwa wagombea 12, waliorejesha fomu jana kugombea ubunge katika jimbo hilo. Mwakalebela anagombea Jimbo la Iringa Mjini ambalo kwa sasa linashikiliwa na Monica Mbega.

Udiwani Bunda

Joseph Malimbe

Arusha warejesha fomu kimya kimya

Wagombea ubunge kwa tiketi ya CCM waliochukua fomu za kugombea ubunge Mjini Arusha, wamerudisha fomu zao katika ofisi za wilaya hapa mjini kimya kimya. Miongoni mwa waliorudisha fomu hizo jana ni pamoja na Dk. Batilda Buriani na Dk. Hamisi Kibola huku wagombea wengine wakiwa bado wanasubiriwa. Wagombea wengine waliochukua fomu na kuzirejesha ni pamoja na Deogratius Mtui, Felix Mrema na Micheal Sekajingo.

Jimbo la Ngorongoro

Mathewtak  Ole  Timan, Saning Ole Telele, Fidelis Ole Kashy, Godfrey Laliya, William Ole Nasha, Pius Sanai, Peter Metele, Vicent Mbirika  na  Patrick Gwedig nako  Wilaya ya Karatu ni John Burra, Dk Lorry na Dk Sixbert.

Jimbo la Monduli

Waziri Mkuu (mstaafu) Edward Lowassa, Dk. Salash Toure, Wilaya ya Arumeru Magharabi ni Goodluck ole Medeye, Elisa Mollel na Thomas Sabaya.

Arumeru Mashariki

William Sarakikya, Anthony Musani, Elirehema Kaaya na Jeremia Sumari.

 

   

Uchaguzi umeanza

*Mgombea akutwa na mguu wa mtu Mbeya
*Ni wa Chadema aliuficha uani, akamatwa

Na Maregesi Paul

MGOMBEA ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika Jimbo Jipya la Makongorosi lililoko Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya, George Mtasha (50), amekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya baada ya kukutwa na mguu wa mtu.

Katika tukio hilo, Mtasha ambaye pia ni mwenyekiti mstaafu wa chama hicho Mkoa wa Mbeya, amekamatwa na mwenzake aliyefahamika kwa jina la Paul Mnyambwa (43).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Adcocate Nyombi, aliiambia MTANZANIA kwa njia ya simu jana kuwa, Mtasha na Mnyambwa walikamatwa jana saa 12.50 alfajiri baada ya polisi kupata taarifa kutoka kwa raia mwema, kwamba watu hao wanamiliki mguu wa mtu.
“Ni kweli kuna watu wawili wakazi Bwawani, Makongorosi Chunya ambao wote ni wafanyabiashara wa madini ya dhahabu, tunawashikilia hapa. Kabla ya kuwatia mbaroni, awali tulipata taarifa kutoka kwa

 

Ubunge ni maajabu

*Fomu ya Dk. Makongoro yakataliwa
*Profesa Wangwe ajitosa rasmi Kibaha
*Mbunge wa EAC anagombea udiwani
*Serukamba apeta, Wassira wampima
*Dar yavunja rekodi, soma orodha yote

Na Waandishi Wetu


WAGOMBEA 38 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wamejitokeza kuchukua fomu za kuwania ubunge katika Wilaya ya Kinondoni, yenye majimbo matatu ya Ubungo, Kawe na Kinondoni, kati ya majimbo hayo Jimbo la Ubungo linatarajiwa kuwaka moto.

Mchuano mkali unatarajiwa kujitokeza kwa baadhi ya wagombe ubunge ambapo Nape Nnauye na Shamsa Mwangunga wanatarajia kuumana vikali ndani ya chama huko Ubungo, huku wakikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mgombea ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika.

Katika hali isiyo ya kawaida, mgombea mmoja wa ubunge anayewania Jimbo la Kinondoni, Mateo Kanela, jana aliwashangaza baadhi ya viongozi wa ofisi za CCM, wilaya ya Kinondoni, baada ya kushindwa kutaja namba ya kadi yake ya uanachama kwa madai kuwa kadi ameisahau nyumbani.

Akizungumza wakati anahojiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Godfrey Tondo, ambaye pia ni Katibu wa chama hicho wilayani hapo, Kanela alisema: “Siyakumbuki majina ya viongozi wa chama changu kwa sababu huwa sikai Dar es Salaam nakaa Kahama.

“Nikipata kazi hii ya ubunge nitaanzisha kiwanda, kwa sasa hivi nafanya biashara ya kuuza duka Magomeni. Nimeidhinishwa na Serikali, naamini kuwa sina kipingamizi katika jimbo hili, nina hakika nitapita, kwani Serikali imeniidhinisha yenyewe.”

Wagombea ubunge waliojitokeza katika Jimbo la Ubungo ni Nape Nnauye, Dk. Apollo  Kissai, Slaus Mwishemba, Kanali Gaspar Hiza, Alfred Nchimbi, Peter Msuya, Hawa Mg’humbi, Assumpta Nalitolea, Michael Lupiana, Perpetua Haule, Eliona Nkya na Shamsa Mwangunga.

Jimbo la Kawe

Faustin Kikove, Mahamoud Madenge, Nicodemus Chengula, Eric  Suma, Omari Wahure, Biton Mwenisongole, Harold Maruma, Dk. Malima Bundara, Jumaa Pijei, Margaret Lema, Japhet Robi, Angela Kizigha, Dk. Petronilla Ngiloi, Elias Nasera, Zainuddin Adamjee na Kippi Warioba.

Jimbo la Kinondoni
Iddi Azzan, Mustafa Muro, Kakolwa Mbano, Shy-Rose Bhanji, Issa Omary, Godwin Kabisa, Mpoki Mwambulukutu, Bakari Maige, Mateo Kanela na Mackdonald Lunyilija.

Waliochukua fomu za Ubunge Viti Maalumu Mkoa

Zarina Madabida, Tatu Malyaga, Margaret Kimambo, Grace Mtesigwa, Amina Israel, Mossy Mbwando, Hadija Kopa, Joyce Kajula na Nuru Kaku.

Waliochukua fomu za Udiwani Viti Maalumu Wilaya ya Kinondoni tarehe 19/7/2010

Jimbo la Ubungo

Sophia Fitina, Joan Mazanda, Elukaga Minango, Angela Mfinanga, Asnath Mambo, Florence Masunga, Tatu Mnekeya, Angela Halla, Theresia Chihota, Zuena Abdallah, Grace Kabigi, Salama Lusogo, Ningile Kapange, Ester Mkandawile, Omega Masawe, Nuru Kaku na Rehema Mayunga.

Jimbo la Kawe

Hilda Rwebangira, Kulthum Sagamiko, Everly Hatibu, Bernadette Ritti, Mwanaisha Sudi, Rozina Urio, Renata Semitende, Julia Hoza, Leah Onyango, Asha Majura na Basilisa Sawere.

Jimbo la Kinondoni

Grace Mwashala, Hilda Rwezaura, Kimwana Sherally, Lilian Mchaa, Florence Ndege, Subira Kondo, Huba Hassan, Tiba Hamisi na Fatma Salim

Kwa upande wake, aliyekuwa Mbunge wa Ukonga, Dk. Makongoro Mahanga (CCM), fomu zake zimekataliwa na Katibu wa CCM, Wilaya ya Ilala, Haroun Mkalimoto, baada ya mbunge huyo kushindwa kujaza kipengele kimoja katika fomu hizo.

Fomu hizo zilikataliwa jana saa 6.17 mchana, baada ya Dk. Mahanga kuziwasilisha kwa Katibu huku zikiwa hazikujazwa katika kipengele anachotakiwa kusaini Katibu Mkuu.

Kabla ya tukio hilo lililoonekana kuwashangaza waandishi wa habari waliokuwa ofisini hapo, Dk. Mahanga aliingia ofisini hapo kwa mbwembwe huku akimtania mmoja wa wagombea wa Jimbo la Ukonga, Brighton Mzungu, aliyekuwa akichukua fomu ya kuwania jimbo hilo.

“Jamani safari hii Jimbo la Ukonga linagombewa kama mpira wa kona, haya bwana, kila la kheri,” alitania Dk. Mahanga.

Alipomaliza kusema hayo, Dk. Mahanga ambaye juzi alichukua fomu za kugombea ubunge katika Jimbo la Segerea, alikaa kwenye kiti na kuwasilisha fomu hizo kwa Katibu wa Wilaya ya Ilala.

Baada ya Katibu kuzipitia, aligundua kuwa, nafasi ya Katibu Mkuu ambayo inatakiwa kusainiwa na Katibu wa Tawi aliloko mgombea wa ubunge, ilikuwa haikujazwa.

“Kwa hiyo, nenda ukarekebishe kasoro hii maana muda bado upo,” alisema Mkalimoto na kumfanya Dk Mahanga aanze kumpigia simu Katibu wake wa tawi ili waone namna ya kusaini sehemu hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya tukio hilo, Mkalimoto alisema utaratibu wa kuwarudishia wagombea fomu zao na kuwataka wakarekebishe kasoro zilizoko ni wa kawaida kwa kuwa muda wa mwisho wa kupokea fomu haujafika.

Hadi kufikia jana mchana, wagombea 26 walikuwa wamechukua fomu kugombea ubunge katika majimbo matatu yaliyoko Wilaya ya Ilala ambayo ni Ukonga, Sgerea na Ilala.

Jimbo la Ukonga

Injinia John Kengere, Kamishna (mstaafu) Aziza Mursali, Manga Selelya, Isaya Christabela, Hamza Abdallah, Chacha Wambura, Godwin Barongo, Magesa Magesa, Sande Mnozya, Beatrice Moses, Eugen Mwaiposa, Ramesh Patel na Brighton Mzungu.

Jimbo la Ilala

Ni aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Mussa Hassan Zungu, Jafari Juma, Juma Chikoka na Blandina Mluzya.

Jimbo la Segerea

Dk Makongoro Mahanga, Salusian Kato, Kiomon Kibamba, Glorious Luoga, Zahoro Yasuka, Paul Mahodo, John Jambele, Joseph Kessy na Venance Victor.

Waliorejesha fomu hadi kufikia jana katika Jimbo la Ukonga ni Mwaiposa na Manga Selelya. Ilala ni Zungu na Jafari Juma, wakati Segerea ni Kessy, Luoga Kato na Dk Mahanga ambaye fomu zake zilikataliwa.

Katika hatua nyingine, Mkalimoto alisema leo jioni wagombea wote watakuwa na kikao cha pamoja kupewa masharti ya kushiriki uchaguzi huo.

Hadi kufikia jana alasiri wanachama 26 walikuwa wamechukuwa fomu za kuwania  ubunge, ambapo 16 watawania Jimbo la Kigamboni, akiwamo mbunge mtetezi wa jimbo hilo,  Abdulrahiman Msomi na aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Temeke kipindi cha awamu ya tatu, John Kisabo, wakati Jimbo la Temeke waliochukuwa fomu ni 10.

Jimbo la Kigamboni

Joseph Ngwasho, Dk. Faustine Dungulile, Mariam Kambi, Issa Mohamed, Ahmed Shabani Mbegu, Briggen Haroon, Amindi Kichilingulo, Siaga Kiboko, Phares Magesa, David Shaba, Thadeus Musembi, Mwinchoum Abdulahman Msomi (mbunge wa sasa), Athuman Mbwana, Petter Gabriel, Enock Temu, John Kibaso na Pius Joseph.

Jimbo la Temeke

Ni Mbunge wa Jimbo hilo, Abasi Zuber Mtemvu, Benedicto Likwembe, Hadija Kasola, Amani Johnson, Salum Khamis Salum, Mohamed Msham, Richard Tambwe Hizza, Mohamed Nassoro Nondo, Peter Nyalali na Inayat Mohamed.

Jimbo la Muleba Kusini

Waliochukua fomu ni Mkurugenzi wa Shirika la Makazi Duniani (UN-HABBITAT) Profesa 
Anna Tibaijuka, mbunge wa sasa Wilson Masilingi na Kamishina (mstaafu) wa Polisi Alfred Tibaigana.

Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki

Naye mgombe wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Mzeru Paulo, ameiomba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU)  kuhakikisha inazuia mianya ya rushwa ambayo inaweza kujitokeza kwa wagombea mbalimbali hapa nchini.

Jumla ya wagombea 11 wamejitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki ambao ni yeye Mzeru Paul, Amani Kondo, Jamila 
Mohamed, Salumu Makwaya, Semindu Pawa, Gabriel Mkwawe, Amani Mwenegoha, Lucy Nkya, Kassim Hegeka na John Nkundi.

Uwakilishi Zanzibar

Waliochukua ni Naibu kiongozi ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Ali Juma Shamhuna (Donge), Waziri wa Kilimo, Mifugo na Mazingira, Burhani Haji 
Saadati (Kikwajuni), Hamza Hassani Juma (Kwamtipura), aliyekuwa ameshikilia wizara iliyopo chini ya Waziri Kiongozi, Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Machano Othman Said (Chumbuni), na Waziri anayeshughulikia Fedha na Uchumi, Dk. Mwinyihaji 
Makame (Dimani).

Mawaziri wengine waliojitokeza ni pamoja na Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ, Suleiman Othman Nyanga (Jang’ombe), Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na 
Ardhi, Mansoor Yussuf Himid, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Sultan Mohamed Mugheir (Mji Mkongwe) na Waziri Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha (Mwanakwerekwe).

Makada wengine waliojitokeza kuchukua fomu za uwakilishi ni pamoja na Ali Denge Makame (Amani), Kamal Basha Pandu, (Rahaleo), Ibrahim Ali, Abdullatifu Jusa Sadiq (Amani), Sharrif Shashi (Chumbuni) Perera Ame Silima (chumbuni) na Simaio Mohamed Said (Mji Mkogwe).

Wengine waliojitokeza kuchukua fomu hizo za Uwakilishi ni Asma Ali Mussa (Kwamtipura), Nassor Salum Ali, Enzi Talibu, Zaharani (Rahaleo), Ali Salum Haji (Kwahani), Mussa Khamis 
Silima (Uzini), Sharifa Abeid Salum (Koani), Bimkubwa Khamis Janja na Mshihiri Ali Faki (Fuoni), Issa Haji Issa (Chwaka) na Omar Gulam (Dole).

Ubunge Zanzibar

Wanachama walijitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi ya Ubunge ni pamoja na Waziri Ulinzi na Usalama Dk. Hussen Mwinyi (Kwahani), Ameir  Haji (Magomeni), Kanal Fara (Rahaleo), Mussa Hassan Mussa (Amani), Parmuki Hogan Sing (Kikwajuni) na Ali Abeid Khamis (Kwamtipura).

Wengine ni Issa Khamis Issa (Mpendae), Ali Hassan Omar (Jang’ombe), Salehe Ramadhani Ferouzi (Kikwajuni), Omari Said Ameir (Mpendae), Dk. Ahmada Hamad Khatib (Koan), Mohamed Muhsin Simba (Fuoni), Sylvester Massele Mabumba (Dole), Alsha Si Said  (Kwamtipura), Rahma Rashid (Magomeni) na Abdalla Mabodi (Rahaleo),

Viti Maalum Mkoa wa Dodoma

Waliochukua fomu hizo ni Mbunge wa sasa wa Viti Maalum, 
Felister Bura, Mary Chihoma, Catherine Ndahani, Christina 
Cylil, Sara Mwaga, Maram Mfaki, Salome Kiwaya, Stella Fweda na 
Mary Mbogo.

Wengine ni Dk. Salma Chande, Catherine Mgogoro, Juliana 
Manyerere, Dokilia Bashemeko, Winfrida Andrew, Edna Ndejembi 
na Rachel Temba.

Jimbo la Mpwapwa

Mbunge anayetetea jimbo, George Lubeleje, Gerigori Teu, Yona Mtema, David Lusa, Dk. Mombo Kamwaya na Rehema Harahara.

Jimbo la Kibakwe

Mbunge anayetetea jimbo George Simbachawene, Paulo Geyanga, Dk. Federick Kasanga, Omari Tuwakali, Lawrian Ndimbo, Solomon Mgiliule na Akrey Muyanga.

Jimbo la Dodoma Mjini

Hadi jana mchana walikuwa wameongezeka wanachama wawili, akiwemo mbunge wa sasa Ephraimu Madeje na Reginald Mavere. Wanachama hao wamefanya idadi ya waliouchukua fomu katika jimbo hilo kufikia 14.

Jimbo la Kibaha Mjini

Dk. Zainabu Gama (mbunge anayemaliza muda), Silvester Koka, Charles Makunga, Hamis Masasa, Dk. Rose Mkonyi, Profesa Samweli Wangwe, Eusibius Mvuoni na Kibindu Yohane.
 
Nafasi za madiwani Viti Maalum kupitia (UWT) mpaka sasa fomu zimechuliwa na wagombea 15 akiwemo Mwandishi wa Habari wa Uhuru na Mzalendo, Selina Wilson. Udiwani kupitia kata  wamefikia 40.
 
Katibu  wa CCM Mkoa wa Pwani, Sauda Mpambalioto, alisema kuwa mpaka sasa kuna jumla  wagombea wa nafasi ya ubunge 47 ikiwemo Rufiji (saba), Mafia (watano), Kibiti (saba), Kisarawe (wawili), Chalinze (watano), Mkuranga (watatu) na Bagmoyo (watatu) huku kundi la umoja wa Vijana  waliojitokeza ni wanne.

Udiwani Tanga

Mkulima maarufu wa Chai wa Kijiji cha Nkelei kilichopo Kata ya Tamota, wilayani hapa, Bakari Banda (70) amechukuwa fomu ya kugombea Udiwani katika Kata hiyo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi.

Mhifadhi Samaki aina ya Silikanti (Kishapu) na Katibu wa Umati 
Wilaya ya Tanga, Mwanaisha Shabani, ametangaza nia ya kuwania 
udiwani viti maalum tarafa ya Chumbageni Tanga.

Viti Maalum UVCCM

Ofisa Habari wa Tume ya Kudhibiti Ukimiwi Tanzania (TACAIDS), Gloria Mzirai, ametangaza nia ya kugombea ubunge wa Viti Maalumu kupitia Jumuiya ya Umoja wa Vijana, UVCCM Mkoa wa Morogoro. Amechukua fomu jana.

Jimbo la Karatu

Dk. Wilbald Lorry
 
Huko Singida

Aliyekuwa mkuu wa wilaya katika wilaya mbalimbali hapa nchini, Hawa Ngulume, amekanusha vikali uvumi ulioenea kuwa ametumwa na Waziri Mkuu (mstaafu), John Malecela kugombea ubunge katika Jimbo la Singida Mjini.

Kutoka Kigoma

Aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa tiketi ya CHADEMA, Kitita Magonjwa, amekihama chama hicho na kuchukua fomu ya kuwania udiwani wa Kata ya Rusimbi kwa tiketi CCM jimbo la Kigoma Mjini.

Katika hatua nyingine, jumla ya wanachama watatu wa CCM wamechukua fomu kuomba kuteuliwa kugombea ubunge kupitia chama hicho katika Jimbo la Kigoma Mjini, akiwemo Mbunge wa sasa jimbo hilo, Peter Serukamba. Wengine waliochukua fomu juzi ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM Wilaya Kigoma Mjini, Nashon Bidyanguze na Mhasibu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Adam Mgoi.

Jimbo la Muhambwe

Felix Kijiko, Jamal Tamim, Emanuel Bwegenyeza, Brighton Gwamagobe, Richard Kigaraba, Barakabise Mbogoyo, Dk.Chrispine Shami, aliyewahi kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Arcado Ntagazwa, Regina Kayabo na Salome Choma.

Jimbo la Buyungu

Hadi tunakwenda mitamboni Naibu Waziri wa Kilimo na Umwagiliaji, Christopher Chiza pekee ndiye aliyechukua fomu katika jimbo hilo.

Jimbo la Mvomero

Marcus Mgweno, Amos Makalla na Sadiq Murad

Moshi Mjini

Justin Salakana

Jimbo la Arumeru Magharibi

Loy Thomas Sabaya na Robinson Meitinyiku.

Jimbo la Arumeru Mashariki

William Sarakikya na Anthony Musani.

Jimbo la Arusha

Mbali na Dk. Batild Burian aliyechukua juzi, jana ameongezeka mbunge wa Jimbo hilo, Felix Mrema.

Jimbo la Ngorongoro 

Mathewtak Ole Timan, Saning' Ole Telele, Fidelis Ole Kashay, Godfrey Laliya, Williamu Ole Nasha, Pius Sanai,Peter Metele, Vincent Mbirika, Patrick Gwedig.

Jimbo la Bunda

Tembe Nyaburi, Emmanuel John Phales, Ginche Kisase, Yeremia Kulwa Maganja, Samwel Mgaya Tumaini, 
Jeremiah John Wambura na Stephen Wassira.

Jimbo la Mwibara
Kangi Alphaxad Lugola, Bartazar Ryamongo, Mtangazaji wa Channel Ten, Cyprian Msiba, Chrphord Kajana, Emmalieza Chilemeji, Bitulo Paschal Kazeli na mwanamke pekee ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi, Bahati Misana.

Jimbo la Simanjiro

James ole Millya, Christopher ole Sendeka (mbunge anayemaliza muda) na Lewnganasa Soipey.

Udiwani Dar es Salaam

Mbunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki, Dk. Didas John Massaburi, ametangaza nia ya kugombea udiwani kata ya Kivukoni kwa tiketi ya CCM.

Mchakato wa kuchukua fomu hizo na kurudisha unaendelea mpaka leo kabla ya saa 10:00 jioni ambapo kampeni zitaanza kupigwa Julai 22 hadi 28 ndani ya chama na kura za maoni kwa 
wagombe zitapigwa Agosti Mosi katika matawi yote ya CCM.


Habari hizi zimeandikwa na Waandishi Wetu, Maregesi Paul, Mussa Katuga, Herrieth Benny, Audax Mutiganzi, Rose Chapewa, Grace Shitundu, Rachel Mrisho, Debora Sanja, Gustaphu Haule, Sussan Uhinga, Rose Chapewa, Prisca Libaga, Nathaniel Limu, Iddi Risasi, Eliya Mbonea, Ahmed Makongo, na Mwanaidi Abasi wa DSJ.

   

Page 1 of 23

More Latest News

  • 1
  • 2
  • 3
  • 4

cartoons



Who's Online

We have 7 guests online

Login Form